Never Again! Fixing Electrical Fittings Inside a Hot Ceiling in Makueni

Leo nimejua kuna jobs zingine ni za watu wa roho ngumu! Nilipata deal ya 15K kufix electrical wires kwa ceiling ya flat roof (ya mabati) moja hapa Makueni. Nikaingia kwa ceiling thinking ni kazi rahisi—my friend, si ni sauna huko ndani! Joto ilikuwa ya kuchemsha akili, jasho linatiririka mpaka kwa macho, halafu hakuna hewa hata kidogo. Kila nikivuta pumzi, ni kama naingiza moto kwa mapafu. Alafu dust—ni kama miaka yote hakuna mtu ameweka macho huko juu. Nilikuwa natema vumbi kama nimekula mchangarawe. Hapo ndio nikaona spiders wakubwa wanatembea kwa corners, wengine wanaangalia tu wakijiuliza huyu mgeni anafanya nini hapa.

Nikiwa halfway fixing some junctions, nikaweka kichwa vibaya nikagonga truss ya chuma. Ilibidi nishike kichwa for like 30 seconds, nikijiuliza kama hii pesa ni worth it. Hadi simu yangu ikasema "Overheating, shutting down." 😭 Ilibidi nimazishe kazi haraka, jasho likitiririka, mwili umeshikana na vumbi kama mkate ya boda boda. Baada ya 6 hours, nilishuka chini, nikaangalia mwenye nyumba nikamwambia, "Job imeisha, lakini hii ndio mara ya mwisho naingia kwa ceiling ya flat roof." 15K ilikua tamu, but siwezi rudia hii kazi!